XClose

UCL Anthropology

Home
Menu

Episode 3: Know your rights Swahili Transcript

Nakala – Sehemu Ya 3

Mhoji: Hein Aung Htet
Mhojiwa: Eva Maria Anyango Okoth

Hein: Habari na karibu kwa ‘Kusikia juu ya kishindo’ podikasiti ya mfululizo ya sehemu tatu ambayo ina ondoa utata katika sauti inayo endelea ulimwenguni juu ya ujenzi wa bwawa kubwa katika Afrika Mashariki. Katika mfululizo huu, tutachunguza maana ya hii sauti kwa watu wanaoishi katika njia yake. 
Mimi ni Hein Aung Htet na kwa sasa ni mwanafunzi wa anthropolojia katika chuo kikuu kishiriki cha London. Katika sehemu yetu ya tatu na ya mwisho kwa mfululizo huu, tutakuwa tukijadili masuala ya haki ya kimazingira katika Afrika Mashariki, kwa kuangalia ni kwa namna gani jamii  hutumia sheria na uanaharakati wa kisheria kutetea haki zao katika uso wa miradi mikubwa ya ujenzi. Nina maslahi maalum kwenye mada hii usuli wangu ukiwa umetoka Burma ambako sheria za kimazingira bado hazijawa halisi sana hali ambayo inaathiri kwa ukali wakaazi na riziki zao. Hii imesababisha vurugu za kisiasa ambazo zingeweza kuzuilika kwa urahisi. 
Nitakuwa nikizungumza na Eva Maria Anyango Okoth, mwanasheria na Afisa Mwandamizi wa programu aliyeko shirika lisilo la kiserikali, Haki ya Asili. 

Hein (katika mahojiano): Habari ya asubuhi kutoka hapa London. Sijui ni saa ngapi huko Kenya muda huu lakini vipi? 

Eva: Samahani. Ni muda wa chakula cha mchana. 

Hein: Ah, habari za mchana. Kwa hiyo unaendeleaje leo? 

Eva: Naendelea vizuri. 

Hein – Simulizi Ya Sauti


Tulipoanza mfululizo huu wa matukio, lengo letu lilikuwa ni kuzingatia mradi wa Kiwanda cha Umeme wa Maji wa Julius Nyerere uliyoko kusini mwa Tanzania, mradi wenye utata ambao, utakapokamilika, utaweka bwawa katika Mto Rufiji, kimsingi utasumbua mfumo wa ikolojia na riziki za wakaazi 200,000 chini ya mkondo wake. Mashirika yasiyo ya serikali ya kimataifa yenye ofisi Tanzania, pamoja na viongozi wa upinzani serikalini na wasomi wazawa wamelaani mradi kuwa ni janga la kimazingira na kijamii.  

Katika sehemu ya 1, tulisikia kuhusu usuli na mktadha wa kihistoria ya bwawa hili, na katika sehemu ya 2 tulisikia kuhusu namna wazawa wa Tanzania wanaweza kuwa au kutokuwa na sauti katika utumiaji na usimamizi wa maji.   Tulitumaini kusikia moja kwa moja kutoka kwa wazawa katika mfululizo huu, lakini kutokana na mvutano wa kisiasa kuhusiana na mradi, imekuwa ngumu kupata Watanzania walioko tayari kuzungumza nasi. Mwishowe, haijaonekana kama ni salama au wajibu wetu kualika wazawa kwenye podikasiti kwani wangeweza kukutana na matokeo hasi toka kwa mamlaka.  

Lakini tuna furaha tumeweza kuzungumza na Eva, anayeshirikisha utambuzi wake na uzoevu wa kufanya kazi na jamii ya wazawa katika nchi jirani ya Kenya. 

Eva anaishi Nairobi, ambapo kazi yake imeelekezwa kutetea mazingira na haki za binadamu za jamii zilizotengwa. 

Anafanya kazi kuhakikisha jamii za wazawa wana sauti katika miradi ya maendeleo. Pia, anasaidia utekelezaji wa sheria iliyowekwa katika katiba ya Kenya kwa ajili ya mazingira masafi na yenye afya, ufikiaji wa taarifa na haki, na kushiriki katika michakato ya maamuzi. 

Ingawa Eva hatazungumza nasi kipekee, kuhusu umeme wa maji leo, maarifa yake na uzoevu ndani ya Kenya hutupa utambuzi katika miradi ya maendeleo ndani ya Afrika Mashariki na changamoto zinazopatikana ili kuhakikisha jamii za wazawa zinasikilizwa.  Uzoevu wake unatokana na miradi ya kujenga viwanda vya mafuta ya kisukuku, na zingine sambamba zinatokana na uendelezaji wa umeme wa maji Tanzania na nchi zingine pia. 

Eva alinieleza kuwa ingawa kuna sheria za kulinda mazingira na jamii za wazawa nchini Kenya, mara kwa mara hakuna uwezo au uwajibikaji wa kutekeleza sheria hizo. Na hapo ndipo kazi yake na mashirika ya Haki ya Asili inapokuja.  

Tunashukuru sana Eva kwa kuzungumza nasi! 

** Mahojiano Yanaanza

Hein (katika mahojiano): Hivyo swali la kwanza ninataka kukuuliza ni, nini kilichokuharakisha kuingia katika haki ya mazingira kote katika mfumo wa sheria? Ni kwa nini mfumo wa sheria na ni nini kilichokuvutia kuhusu fani hii? 

Eva: Hivyo kwangu, kilichonihamasisha ni kipengele cha uwezekano wa kutafuta njia ya kufanya sheria ifikike kwa watu wa kawaida ambao mara nyingi wanateseka kwa ajili ya, unajua, ukiukwaji wa haki zao za kibinadamu kwa sababu ya ukosefu wa uelewa wa hizi haki na namna ya kuzidai. Hivyo, siku hizi kwa mimi, nipe hiyo fursa ya kuweza kufanya sheria kuwa ya kidemokrasia na kusuluhisha masuala. 
Hein (katika mahojiano):  vitu vipi baadhi ambavyo unajaribu kusukuma kuhusu wazawa, haswa kama mwanasheria wa Haki ya Asili? 

Eva: Hivyo kwa mtazamo wa haki ya asili, tunachojaribu kuisukuma ni wewe kujua, jamii faidika na msaada, raia wa kawaida na wakala, wanahitaji waweze kudai huu uwajibikaji na uwazi. 

Hivyo kama nitaweza, nitatoa mfano wa namna hii ambayo imetokea, ni tukio tuliofanyia kazi, linaloitwa tukio la kiwanda cha Lamu aliyeitwa. Ni mfano mzuri sana kwa sababu serikali ya Kenya ilipopendekeza kiwanda chetu cha kuchoma makaa ya mawe, katika video hii, katika maeneo ya kijijini, jamii huko muda ule, hawakuelewa kilichokuwa kinaendelea, na labda hawakuwa na faida kutokana na kuijua sheria na namna ya kuitumia kudai uwajibikaji.  Lakini katika mazingira ya kisheria iliyoanza kutendeka toka muda, ungeweza kuona mabadiliko chanya kuhusu namna gani wanavyoshiriki katika michakato hii. Na kwa tukio hili, jamii zilizo nyingi waliweza kudai taarifa kwa miradi hii. Tuliweza kufanya kazi pamoja kushiriki katika michakato ya somo la tathmini ya athari za kimazingira, ambapo waliuliza maswali, kutoa dukuduku zao kuhusu athari za mradi huu zinazoweza kutokea. Na kwa kuwa hawawezi kupata uwajibikaji waliotaka, ndipo jamii walikwenda mahakamani kutafuta na kudai, uwajibikaji, na hii kwa hakika ilifanikiwa. 

Hein: Unaweza kutupa mfano wo wote wa kazi yako hapo Kenya au ni kwa namna gani vikundi vya wazawa yanaweza kujipanga kuahirisha au kuzuia miradi mikubwa ya kimiundombinu, pengine miradi ya msingi na vikundi vya wazawa?

Eva: Ndiyo. Ndiyo, hakika. Anzia tu nilipo achia, kwa sababu somo moja tulilojifunza kutoka mradi wa kiwanda cha kuchoma makaa ya mawe Lamu ni kwamba kuna nguvu nyingi kutoka kujipanga kwa wazawa. Ni muhimu sana kutoka neno, nenda kwa jamii ziweze kuja pamoja, kujipanga na, unajua, kuweka mbele msimamo wa kawaida kwa namna wanavyohisi na wanavyofikiri kuhusu aina hizi za maendeleo yaliyokuzwa na yanayopendekezwa katika maeneo yao. Na kama ninanvyokumbuka, kitu kimoja kilichofanyika walipoanzisha tukio ni kwamba jamii zilikuja pamoja na kuanzisha shirika mwamvulli ambalo lilileta pamoja vikundi tofauti vya watu katika jamii wakiwepo wanawake, vijana, wazee, kupitia shirika hili lililojikita katika jamii linaloitwa Save Lamu na hivyo shirika hili mwamvuli ndilo lililoweza kuwa mbele ya pambano la kupinga mradi.

Kulikuwa pia na harakati ya kitaifa iliyoanzishwa iliyoitwa ondoa ukoloni. Hivyo harakati hii inakuza wataalam wanasheria waweze, unajua, kusemea suala hili katika ngazi ya kitaifa kwa sababu suala hata kama haliathiri jamii moja kwa moja, pia lina athari katika ngazi ya kitaifa, ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja.  Hivyo, kwa mimi, kujipanga kwa jamii hakika ilikuwa tukio lililoleta badiliko. 

Hein (katika mahojiano): Kama ujuavyo, pale podikasiti yetu ilielekezwa  kwa mradi wa umeme, umeme wa maji vile vile. Hivyo unatoa mfano wa namna kama, kama kuna mifano yo yote Kenya kama vile, vikundi kujipanga dhidi ya miradi mikubwa ya umeme wa maji?

Eva: Hivyo likija suala la mradi wa umeme wa maji, siwezi kuzungumzia kwa uwazi tukio maalum tuliofanyia kazi, lakini kwa ujumla kwa mimi, kinachoingia kwenye akili yangu ni huu mjadala tu kuhusu mabadiliko ya nishati, unajua, ambapo jamii nyingi nyingi hujielekeza kutumia nishati inayoweza kutengenezwa upya ambayo si haba. Yenye hatari haba na isiyo changia ukosefu wa haki ya hali ya hewa tunayoona. Hivyo likija suala la aina hizi za majadiliano wa miradi, na ilishakuwa, ndiyo, tunahitaji kubadilika kutumia nishati inayoweza kutengenezwa upya, iwe umeme wa maji, iwe jotoardhi, hata hivyo, zinatafsiri mabadiliko yatakuwa tu hivyo, inamaanisha kuwa hata unapoanzisha aina hii ya miradi, basi utii wa kanuni za kimazingira na kuhakikisha kuwa wadau husika wanahusishwa katika mchakato, bado litakuwa muhimu sana.  
Hein (katika mahojiano): Kujipanga ina hatari kama vile, kwa jamii za wazawa. Tunajua kuwa mazingira na watetezi wa kimazingira hukabiliwa na migogoro ya kisiasa, hivyo ni kwa namna gani watetezi wa kimazingira wa kiafrika wanafanya kazi ya kujisaidia?

Eva: utaona katika baadhi ya takwimu zinazo tolewa kuwa, kwa kila kiwango cha mashambulizi, idadi ya matukio zinaongezeka kwa njia inayo tia wasiwasi sana. Nitaanza na moja ya mwaka uliopita. Mnamo 2021 mwaka uliopita, ‘Global Witness’ ilitoa ripoti angalau watetezi wanne wanauawa kila siku. Na ninafikiri huu ni mwenendo unaotia hofu kusikia katika takwimu katika bara la Afrika. Siyo matukio mengi kama haya yameripotiwa lakini haimaanisha hayatetewi. Kuna matukio mengi kama haya tulioshuhudia ambamo watu huuawa. Watetezi wa kimazingira waliojiweka nje wanashambuliwa hadharani, hata katika majukwaa ya kidijitali. Katika matukio mengine, kuna uonevu mwingi wa kimahakama na utaona wengi wanafanyiwa, unajua, michakato ya kimahakama ambayo inawakatisha tamaa kiukweli. Kama itakuwa, inawezekana una au una namna ya kesi ya kimkakati dhidi ya namna ushiriki wa umma unavyotumiwa dhidi ya washtakiwa unaowajua, kufungiwa au kufungiwa haki ya jinai au michakato ya haki za raia. Hivyo nafikiri hatari ziko juu. Na sababu ya hii ni kuwa miradi mingi ya maendeleo kama hii kwa hakika zinatetewa na wanasiasa au, unajua, na watu wenye pesa nyingi na hivyo kwa hakika inaenda kuwaletea namna ya hatari.   

Hivyo kwetu, tuna Haki ya Asili, tumeanzisha mradi wa watetezi wa kimazingira wa Afrika, ambayo kimsingi imekusudiwa kutoa mshikamano na msaada muda wo wote, masuala haya yakitokea, labda kwa kutoa tu taarifa kidogo kuhusu namna inavyofanya kazi. Tuna mfuko wa dharura, iliyokusudiwa kuwa utaratibu wa hitikio la haraka kuwasaidia washtakiwa ili wajiondoe katika hatari watakapo patwa na tishio. Na hivyo tutatoa hitikio la haraka kwa namna ya matibabu kwa kujikita kwenye shambulio la kimwili.  Pia tunatoa msaada wa dharura wa kiafya ambapo kwa mfano, mtu amekamatwa akitekeleza uhuru wake wa kutembea. Hivyo kwa tukio kama hilo, tunaweza kuwapa mwanasheria anayeweza kukusaidia, unajua, gharama ya dhamana au mwanasheria anaweza kumsaidia mshtakiwa kupata mkopo. Matukio mengine tumewapa miundombinu ya kiusalama ambapo mshtakiwa anafikiri anaviziwa au unajua, faragha yao inaingiliwa kwa njia moja au nyingine.  Hivyo hizo ndizo aina za misaada ya muda mfupi ambazo Mfuko huu wa Hitikio wa Haraka unatoa. 

Halafu la pili, kadri muda unavyokwenda tumegundua kuwa ijapo tunatoa hitikio la haraka, watu wanahitaji iwepo mbinu makini na ya kukinga vile vile. Hivyo kabla dharura haijatokea, tunachoweza kufanya kuongeza uthabiti wa watetezi na si kupunguza nafasi za matukio hayo kutokea? Na hivyo sasa tumehamia kufanya uwezeshaji wa kisheria na kujenga uwezo kwa mfumo wa mafunzo, unajua, kutokuwa na usalama wa kidijitali, mafunzo, kwa mfano, mafunzo kuhusu usalama wa kimwili. 

Halafu cha mwisho, pia inabidi tufanye mengi kuhusu sheria na mabadiliko ya sera ambapo tunatafuta kushawishi sheria itoe ulinzi mkubwa na kutambua jukumu muhimu ambalo watetezi wanafanya likija pambano la haki ya hali ya hewa na haki ya mazingira.  Hitikio langu, kwa kifupi kwa swali lako ni kwamba mktadha hubadilika kweli. Na kuna mahali ambapo kulinga na, unajua, siasa, mazingira ya kisiasa ya nchi yetu, kuna mahali ambapo sheria ya aina hiyo zinakaribishwa, lakini kwa matukio mengine, inakuwa ngumu.  

Nikiweza kutoa mfano mzuri, ndani ya eneo la Afrika Mashariki katika sehemu kama Kenya, hizi kwa kiwango fulani, kiwango kizuri ya demokrasia, naweza kuona utawala wa sheria kwa kiwango kidogo inafanya kazi na inashuhudiwa kwa mfano, Katiba tuliyonayo na hivyo tunao uwezo wa kushawishi watu wawe katika mwelekeo huo katika nchi ingine, kama sasa naweza kutofautisha kama vile Uganda na TanzaniaI nafasi za ujazo kwa nchi hizo zinatia hofu kidogo, kwa sababu ya watu katika jamii na watu wanaozungumza kwa vitisho vingi.  Na kinachovutia ni, nilikuwa tu Uganda mwezi uliopita, na nilikuwa nafanya haya mahojiano na watetezi baadhi ambao wameathiriwa na bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki, na walikuwa wanashirikisha uzoevu wao kuhusu pendekezo linalotolewa kutengeneza mswada wa haki za binadamu. Lakini mtazamo unaovutia kwao ulikuwa ni kwamba sheria hii isingekuwa na umuhimu katika hatua hii. Na ni kwa sababu nchini Uganda, ni wazi, sheria kwa kiwango fulani zinatumiwa kukandamiza watu. 

Hein (katika mahojiano): Naelewa kwa mktadha huo, katika mktadha wangu wa Burma, ambapo watetezi wengi wa mazingira bado wanafanyiwa uhalifu. Kwa kweli, baadhi yao wanakamatwa na kutupwa jela kwa muda kwa kutetea haki za wazawa au makabila madogo na haki za ardhi. Na mfumo wa kisheria ni ngumu sana kuzunguka. Na inachukua muda mrefu sana na inatumiwa tena na tena, kwa sura inayokandamiza wanasheria na makabila madogo wenyewe ili kusiwe na cho chote kitakacho songa mbele. 
Hii miradi mikubwa ya kimazingira kama vile miradi ya mafuta ghafi uliyoyazungumzia, ingewezaje kuendelea licha ya upinzani wa wazawa? 
Na je kuhusu biashara? Hawaoni kuwa kupoteza riziki za asili itakuwa kitu hasi ila hawaoni kuwa ni kitu hasi kwa leo? 

Eva: Ndiyo, Hivyo nafikiri kutokana na kinacho tendeka katika bara katika nchi nyingi, yuko katika hali ambayo tokeo hili  la utamaduni huu wa ubepari unakua kweli na unajua, ni kwamba inapata mifumo unayojua, unayotafuta kuijua, kupata nguvu na pesa kwa ajili ya jamii maalum wakati wengine wanateseka na athari za kubeba mzigo mkubwa sana hivyo nafikiri asili ya kibepari kuhusu namna maendeleo inavyofanyika, kiukweli inapata maana katika nchi, haswa Afrika, na nafikiri, tena, ni kuhusu tu hizi nia za kibiashara, kwa sababu unagundua kuwa mara nyingi nia za kibiashara zinapewa kipaumbele zaidi ya mahitaji ya jamii.

Hivyo nafikiri nitaweka lawama kwa wazo kwenye mfumo wa maendeleo na uchumi kwamba nchi zetu nyingi zinapitisha kwa upofu. Ukiweza kuiweka hii kwenye mtazamo tukiangalia nchi nyingi zilizoendelea kwa sasa, ili usonge mbele, katika mapinduzi wa viwanda, mavuno yalitumia makaa ya mawe na mafuta ya kisukuku kuendelea, sasa zinaikimbia , unajua miradi ya makaa ya mawe na ya mafuta ya kisukuku. Lakini kejeli ni kwamba miradi hii kwa sasa inahamishiwa bara la Afrika bila kukumbuka kuwa zamani imetuonyesha kuwa huu siyo mtindo ambao ni endelevu.  

Na yote yanahusu, unajua, mtindo wa ‘extractivism’ unaohusu kutaka kunyonya rasilimali kwa faida ya watu maalum baadhi kwa ajili ya mazingira, kidogo ni mambo ya zamani yasiyo ya kistaarabu. Mazingira kidogo hayaadhibu, lakini niseme ni fisadi.  Na kwa hiyo aina hii ya ufisadi ndiyo inayodumisha ubepari. Au mfumo wa kibepari tuliouona, ukitekelezwa zaidi na zaidi. Hivyo nafikiri kuwa kweli kuna hitaji la watu kuwa na akili hiyo, kuhamisha akili. Na zaidi viongozi wetu wanahitaji kweli kufikiri kwa makini kuhusu baadhi ya miradi hii ya maendeleo wanazo ruhusu, hivyo hii zaidi ni suala la kimfumo.  

Hein (katika mahojiano): Kwa kuchuma rasilimali au kufanya mradi wa mafuta ghafi nchini Kenya kama hivyo. Ni ipi migogoro ambayo wazawa wamekutana nayo hasa kazini? Wameitikia kwa migogoro au wameitikia kwa namna ya maandamano kwa baadhi ya miradi kama hii?

Eva: Ndiyo, hivyo kwa bomba la mafuta ghafi ya Afrika Mashariki. Jamii zilizo nyingi wameitikia kupitia niseme wanatumia zaidi idhaa zinazopatikana kisheria waweze kutamka hizi haki kwa sababu likija suala la maandamano, likija suala la kutumia uhuru wako wa kujieleza, hizi ni haki ambazo zinalindwa kwenye Katiba. Na hivyo bila shaka jamii wana sababu kuhoji baadhi ya masuala haya yanayotendeka. Hivyo bomba la Mafuta ghafi ya Afrika Mashariki nikitoa ufafanuzi zaidi, ni mradi ambao una kwenda kuendeshwa au una kwenda kulaza mabomba kutoka eneo la visima vya mafuta, nchini Uganda unakwenda kusafirisha nje mafuta kupitia ndani ya Tanzania. Na kwa hivyo kuna idadi ya jamii kando ya eneo hilo la bomba ambazo zitaathiriwa nayo. Kenya utakavyoingilia ni kwamba zitatokea karibu na Ziwa Victoria, ambayo ni rasilimali ya pamoja na athari ambazo zinaweza kutokana na mradi kama vile mafuta kumwagika unaweza kuenea upande wa Kenya pia.

Tumeona matukio ambamo jamii zimetaka kufanya maandamano, lakini hii haija kuwa na mafanikio, unajua, kwa sababu ya udhibiti wa nafasi za kiraia, kama naweza sema. Taratibu, taratibu, walirudishwa nyuma haswa, kila walipojaribu kushiriki katika michakato ya EIA. 

Eva: Kidogo ni mazingira yanayoleta wasiswasi. Na hakuna nafasi ya watu kuingia katika mazungumzo. Kwa sababu ya vitisho vilivyofanyika kwa ajili ya, unajua, kukamatwa ambako kungeweza kutokea mwaka kama uliopita, kulikuwa na ukamataji wa baadhi ya mashirika ya kiraia na watetezi wa jamii waliokuwa wakishiriki katika kuleta changamoto kwa mradi. Mashirika ya kairaia yaliyo mengi wanaogopa pia kuwa kufutiwa usajili kwa sababu tena ya, kuhusishwa na watu waliokuwa wakipinga maendeleo haya. 

Hata ukiendelea kiuchumi unaweza kuhakikisha kuwa mazingira yanazingatiwa na ndhiyo maana tunadai kuwa wazawa wanashirikishwa na wasiwasi wao unazingatiwa wakati maendeleo haya yakipangwa au kutekelezwa.
Ukiangalia unachokiona, sayansi inasema sasa hivi kwa namna ya, kwa mfano, repoti ya hivi karibuni ya IPCC ni kwamba hatuna muda kama, tuko tayari katika hali mbaya ambapo tunahitaji kuweza kupunguza utoaji wetu wa gesi ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi. Tunahitaji kupunguza kiwango ambacho viumbe hai wamepotezwa. Na maendeleo haya yasipozingatiwa, inamaana kwamba tunapoteza. Kwa hakika tupo katika barabara mbaya. 

Hein (katika mahojiano): Asante. Hivyo ningependa kuelekeza mada kwa wazawa sasa na ningeppenda kukuuliza, sana sana kuhusu hali ya wazawa nchini Kenya, na namna wanaathiriwa na maendeleo ya miundombinu. Unaweza tafadhali kutuambia mengi kuhusu umuhimu wa haki za kimazingira kwa wazawa nchini Kenya, ziwe kiuchumi, kijamii au kiroho au hata kidini? 

Eva: Likija suala la haki ya kimazingira kwa wazawa, naweza kuona kuona ufungu namaanisha, miundombinu na namna inavyowaathiri watu, lakina inaacha ardhi zao nyingi ichukuliwe kwa ajili ya au kwa jina la maendeleo au uhifadhi. Hivyo kuna namna wanahamishia ngome pale ambapo tunaona jamii na wazawa wakitengwa kabisa au wanaondolewa kabisa nje ya maeneo yao na nje ya maeneo ya babu zao, ambazo ndiyo yamehifadhiwa zaidi, na viumbe wako kila mahali, viumbe hai wenye afya. Na hivyo, miundo mbinu ina maana kubwa likija suala la, unajua, kutishia haki zao juu ya ardhi yao na juu ya rasilimali zao. Kutoka mtazamo wangu ,suala la ardhi za wazawa hawa imevuka tu hali halisi, uwepo wao katika ardhi ile, una ufungamano wa kiroho wa kula, wana maadili ya kiutamaduni ambayo wanafungamanisha na ardhi zao, na pia maarifa ya kimila ambayo wamehifadhi kwa muda. Lakini mara nyingi, serikali zilizo nyingi au wadhibiti wa mazingira wanaona wazawa kama kitisho kwa viumbe hai au misitu katika nchi, ambacho si sahihi, kwa sababu ukiangalia wazawa, kuna watu ambao wameweza kuhifadhi mazingira, kuhifadhi misitu kwa kutumia njia zao za kimila za kimaisha. Na wanamiliki hii aina maalum ya maarifa, ambayo kwa kiwango kikubwa, husaidia na kuchangia, unajua, kufadhili tabia nchi, masuala tu ya tabia nchi tunayoona na kuchangia kuelekea, kuelekea kuhakikisha kuwa tunaendelea kwa namna ambayo ni endelevu, na tunatumia rasilimali zetu asilia kwa namna ambayo ni endelevu. 

Hein (katika mahojiano): Kenya ikiwa kama nchi yenye utamaduni na bayolojia tofauti tofauti inayotabiriwa kuendelea kwa kasi kwa karne ijayo, umuhimu wa kuhifadhi hiyo ikoje, utofauti, kama kiutamaduni au kibayolojia katika uso wa maendeleo wa kiuchumi?

Eva: Huku Kenya kwa hakika tuna utofauti mwingi. Na hii inazugumza labda kuhusu utofauti wa kiutamaduni na wa kimila. Kuwa, unajua, jamii hizi zilizo nyingi, jamii za makabila, zimekuwa zikifanya. Pale njia zetu za maendeleo haziruhusu jamii waweze kuendelea kutumia hizi tamaduni na njia hizi za maisha, unajua, kama naweza kutoa mfano mzuri ni kwamba tuna jamii ambazo kikubwa in kundi la ufugaji, na zaidi wanaishi njia tofauti kidogo na jamii zingine.  

Ama unajua, mienendo mingine kwa namna tabia nchi inavyotokea katika nchi, ina maana kwamba njia yao ya kuishi inahatarishwa kwa njia moja na hivyo wanaweza kuhitaji kuhamia nchi zingine za kuishi waweze kuendelea kutafutia maisha yao, hivyo ina maana tunaweza kupoteza njia yake au yao, ya kupata riziki zao. 
Mfano mwingine mzuri ni ambao naweza kutoa kwa jamii za wavuvi ambao kwa wingi wapo eneo la pwani. Na unajua eneo la pwani. Hapa ni mahali ambapo athari za tabia nchi pia tena, hutishia riziki za watu kwa kikubwa. Na ambapo hizi hatari zinajitokeza kwa sababu ya miradi ya maendeleo, halafu uvuvi au kuna uwezekano jamii kupoteza riziki zao na hivyo kuhamia njia zingine, ambayo inaweza isiwe endelevu na pia isingeweza kuhifadhi aina ya utofauti tunao uona. 
Kinyang’anyiro cha rasilimali asili na ardhi zinaweza kuleta hali za mgogoro ambapo jamii tofauti, makabila tofauti kwa sasa zinanyang’anyana ardhi na rasilimali asili kwa sababu hakika ardhi kama bidhaa ina kuwa ghali zaidi wakati watu wanafukuzwa kwenye maeneo yao.  Hivyo tukiangalia nchi nyingi Afrika, si Kenya pekee, Nigeria ni mfano mzuri sana ambapo migogoro mikali inajitokeza kwa sababu ya rasilimali asili. Congo-DRC hali ni hiyo. Hivyo aina hii ya utofauti imetishiwa kiukweli, ambapo hatua hazitoshi kuhakikisha kuna haki ya kimazingira. 

Hein (katika mahojiano): Haswa kama makundi ya kikabila kuwa wingi wa wazawa wanatishiwa kwa wazo la kupoteza utambulisho wakati utambulisho umefungamanishwa na ardhi, ambapo kama, ambapo nimeongelea katika mktadha ya Burma tena, kuna vita kwa sasa baina ya makundi ya wazawa.  Na serikali kwa sababu ya mazingira. Na hivyo nafikiri ni muhimu sana kuhifadhi utamaduni na utofauti wa kimantiki. 
Kwa hivyo, swali la mwisho kwa sababu sitaki kuchukua muda wako mwingi. Asante tena kwa njia ya kufanya hivi. 
Haki ya kimazingira ina umuhimu gani kwa demokrasia nchini Kenya? 

Eva: Ndiyo.  Likija upinzani demokrasia, ni kuhusu kujaribu kuhakikisha kuwa watu wana nafasi, unajua, wanashiriki katika kufanya maamuzi, na kuweza kuzungumzia wasiwasi wao kwa uhuru zaidi, na ni nini haki ya kimazingira inatafuta kufikia ni hali ambapo watu wanawekwa katikati mwa utawala wa kimazingira na wasiwasi wo wote, wana anzisha, suala lo lote wanalo anzisha, lina zingatiwa kwa maamuzi ambayo yangeweza kuathiri yanatolewa na viongozi na taasisi za utawala. Na nafikiri kuwa haki ya kimazingira na inakuwa muhimu sana kwa sababu ina hakikisha kuwa kuna uwazi kwa kila kitu kinachofanywa. Kuna uwajibikaji kwa upande, si tu kwa taasisi binafsi, lakini pia, kwa umuhimu, kutoka serikalini kwenyewe, ambako ina paswa kulinda haki zao. Hivyo, inafanya haki ya kimazingira ambayo ni muhimu kuhakikisha kuwa uwazi na uwajibikaji una shikiliwa.  

Katika mtazamo huo sasa tunaweza sema haki ya kimazingira kiukweli ni nguzo muhimu katika kuleta demokrasia ili kuhakikisha kuwa watu wote wanatendewa usawa na kuwa watu wote wanafurahia haki zilizoko kwenye katiba.  

Hein: Asante sana kwa muda wako, na majibu yako vizuri. Asante sana.

Eva: Kuanzia mwisho wango ilikuwa nzuri kujihusisha juu ya mada hii na kuweza kushiriki, angalau kwa mtazamo wangu, baadhi ya maswala haya na ninatumaini kuwa hii itakuwa muhimu kwa mtu yeyote anayesikiliza.

Hein – Akisi Binafsi
Podikasiti ya leo na Eva ni muhimu katika kuelewa sheria kuhusu ujenzi wa bwawa kubwa na namna ambayo sheria hii inaweza kutumika na nchi kufanya vurugu kwa raia wanaotegemea eneo kwa ajili ya riziki na namna sheria hii inaweza kutumika kunyamazisha wanaharakati ambao huzungumza kuhusu hili. Lakini pia tuliangalia kuhusu namna wanaharakati wanavyotumia sheria kikamilifu kulinda haki za raia. Pia nimefurahia kuongea naye kuhusu athari za ubepari na ukoloni kwa dhana ya maendeleo na namna gani unaleta utata kwani haitumikii nia ya wazawa wanaoishi huko sana sana vikundi vilivyo tengwa.  

Ahsante sana kwa kusikiliza sehemu hii ya mwisho ya mfululizo wetu.  Kama ulikosa sehemu mbili za kwanza, unaweza kuzipata kwenye tofuti, pamoja na nakala ya  Kiingereza na Kiswahili ya kila sehemu. Utapata barua pepe yetu katika tofuti yetu au wasiliana nasi kupitia tweeter kwa anwani: @AnthropoceneUCL  

Tunatumaini tumekupa maana bora ya kinachosukuma shinikizo la mabwawa makubwa na miradi mingine ya nishati katika Afrika Mashariki, na kuvuka kusini mwa ulimwengu.