XClose

UCL Anthropology

Home
Menu

Episode 2: Same river, different uses Swahili Transcript

Podikasiti Ya Umeme Wa Maji – Sehemu 2

Mhoji: Olivia Brown
Mhojiwa: Nathalie Richards

Olivia: Habari na karibu kwa ‘Kusikia juu ya kishindo’ podikasiti ya mfululizo ya sehemu tatu inayo ondoa utata katika sauti inayo endelea ulimwenguni juu ya ujenzi wa bwawa kubwa katika Afrika Mashariki. Katika mfululizo huu, tutachunguza maana ya hii sauti kwa watu wanaoishi katika njia yake.

Mini ni Olivia, na ni mwanafunzi anayesoma Ethnografia, Maandishi na filamu. Katika sehemu ya leo, nitakuwa nikizungumza na Nathalie Richards. Nathalie ni Mshauri wa Kimataifa kwa Wizara ya Maji Tanzania, aliyeko GIZ, Kikundi cha Kijerumani ya Ushirikiano wa Kimataifa. 

[Nathalie na Olivia wanapiga soga]

Ana uzoefu wa miaka mingi kama mtaalam na mtafiti katika fani ya maji, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na sera ya Mazingira. Na alifanya utafiti wake wa masomo ya Uzamivu (PhD) na jamii za kijijini katika Mto Ruaha Mkubwa na Uwanda wa Mto Pangani iliyoko Tanzania

Tunahama kutoka Mto Rufiji na bwawa la Umeme wa Maji la Julius Nyerere katika sehemu hii kuzungumzia zaidi kwa ujumla kuhusu changamoto za kuendeleza sera za haki ya matumizi ya maji katika muktadha wa kiTanzania. 

Kama ni umeme, usafi wa mazingira na maji ya kunywa, au umwagiliaji wa kibiashara, madai ya binadamu kwa maji ni makali na yanaongezeka.  Na mahitaji ya viwanda na watu wa mjini kwa kawaida wanapewa kipaumbele juu ya wale wa vijijini ambao pia wanategemea mito yao kwa kilimo, uvuvi, kuogea na kunywa, na maeneo ya urembo wa asili na umuhimu wa utamaduni.   

Kama Nathalie atakavyotuambia, anavutiwa na namna michakato ya maamuzi kuhusu matumizi ya maji inaweza kuwa ya haki zaidi, kuleta sauti za jamii za vijijini vile vile zile za serikali, wanamaendeleo, na wadau wengine. 

Ijapokuwa watu wa Rufiji hawajapewa fursa ya kushiriki katika maamuzi kuhusu ujenzi na uendeshaji wa bwawa kubwa la Nyerere, tutasikia kutoka Nathalie kuwa vyombo na michakato inakuwepo ili wakaribishwe mezani.  

Oliva: KwaTanzania, matumizi ya maji kimsingi yanadhibitiwa na serikali, ila vikundi vinaitwa Miungano ya Watumiaji wa Maji vinaundwa kuwapa jamii ya wazawa nafasi ya kusema pia.
Nilianza kwa kumwuliza Nathalie kuhusu hii miungano.

Nathalie: Hivyo miungano ya matumizi ya maji zinaanzishwa kwa kuita mikutano ya jamii katika vijiji mbalimbali. Na halafu kuna mchakato wa uchaguzi wa nani atakuwa mwenyekiti, katibu na mhasibu, n.k. Majukumu haya mbalimbali ya miungano ya watumiaji wa maji, na tunachokiona mara nyingi ni aina ya watu ambao wapo kwenye uongozi, tuseme watu wenye baadhi ya aina ya uhalali au mamlaka kuhusu matumizi ya maji, wanaokuja na kujitolea. Ni nafasi ya kujitolea. Kusaidia bodi ya maji katika uwanda kutekeleza mipango ya ugawaji, mipango ya kuhifadhi maji. Na lengo la mwisho kimsingi ni kutumia rasilimali ya maji kwa uendelevu hivyo ni kuhusu nani anapata lini na kiasi gani kwa kweli itolewe. 

Olivia: Kwa kuwa kuingia katika nafasi kwenye Muungano wa Watumiaji wa Maji ni ya kujitolea, wale wanaochukua nafasi wanafanya hivyo kwa uwezekano wa faida na fursa. 

Nathalie: Ni watu ambao wamepata motisha kidogo na pia labda wamepata shukrani ya mamlaka kwa kuwa walisaidia watu kusuluhisha migogoro yao ya matumizi ya maji, n.k. Hivyo kidogo wako makini kuendelea katika ushiriki, lakini pia kidogo ni ushiriki wa kuambatanisha kwa maana kuwa wanajua na hii ni upotovu wa misaada ya maendeleo, pia ni kwamba wanajua kuwa hii miungano ya watumiaji wa maji zinatokana na mawazo kutoka usimamizi jumuishi ya rasilimali ya maji, au angalau mawazo kutoka washirika wa maendeleo.   Hivyo wanatoka Kasikazini mwa ulimwengu, na kuna utegemezi mkubwa wa msaada wa maendeleo kutoka kaskazini mwa ulimwengu. Hivyo dhana ni, kama wanaunga uanzishwaji wa miungano ya watumiaji wa maji, basi kuna nafasi kule ya kuunganisha kwa miunganiko ambayo kifedha ni endelevu zaidi kuliko baadhi ya miunganiko mingine ambayo inaweza kuwa ndani ya jamii, tuseme hivyo kuna wazo hili tukutane tuandae andiko la kuomba fedha.  Tuandiko pendekezo la kupata fedha maalum ya kufanya kazi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kukabiliana, au ufanisi wa matumizi ya maji, n.k. Hivyo kuna tumaini hili kuwa fursa nyingi zitatokana na kujitolea. 

Na, nafikiri watu wengi wanafahamu kuwa kuna kubadilishana katika wanachoweza kufikia na kinachoweza kuwa fursa ya kufikiwa baadaye sana kwa fursa ya uchumi. Hivyo watu wanaelewa hii, mienendo hii mbalimbali inayofanyika kwa wakati maji na kutumaini kuwa kunyakua treni inaweza kuwafikisha mahali penye ufanisi zaidi au fursa nyingi, ila pia kwa wale wenye shauku kuhusu maji. Namaanisha, kuwa pia wapo. Hivyo baadhi wanafanya kwa sababu wanashauku kuhusu mada. 

Olivia: Lakini huu mchakato wa ushiriki wa jamii haina budi kukidhi mahitaji ya watumiaji wazawa wa maji. Kote katika kazi yake ya utafiti, Nathalie amechukua mtazamo muhimu kwa michakato ya kitaasisi, ikiwemo mfumuko wa urasimishaji wa usimamizi wa maji. Nathalie anatambulisha wazo kuwa “kuigiliza kunakofanana”: Serikali au taasisi zikiigiliza sera na miongozo ya utendaji inayotumika katika nchi zingine kwa sababu wanaona kama zimefanikiwa zaidi, ila bila kuzingatia kivipi wako sahihi katika muktadha mpya. 

Nathalie anaona hii ikitendeka ndani ya mifumuko ya michakato iliyorasimishwa ya kuanzisha Miungano ya Watumiaji wa Maji Tanzania. 

Nathalie: hivyo kitu kimoja ambacho kimekuwa kikivutia kidogo ni kuleta tu ufahamu kuwa zoezi la kisanduku cha tiki limekuwa likitekeleza kama zoezi la kuweka tiki kisanduku kwa matukio mengi, na kwamba imekuwepo kwa namna ya uendelevu.  Katika kuanzisha hii miungano ya watumiaji wa maji, kwa mfano, kuna wazo kuwa kisanduku ambamo zinafanyia kazi nadhifu na safi, kama sera ilivyo ila basi fujo kwa biashara ya kila siku ya nini kinafanyika kweli ndani ya hicho kisanduku ndani ya hiyo ofisi.  Kwa sababu ya ucheleweshaji wa fedha na uwezo kimfumo na, n.k. Hivyo ni vigumu kufanya kazi kwa kweli walizopewa, hivyo kwa miungano ya watumiaji wa maji ni vigumu sana kufuata kilichotegemewa kwao kutoka mamlaka ya uwanda na kutoka jamii ambayo watawajibika kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kifedha, uwezo wa kibinadamu, na kiwango cha kazi zinazotakiwa toka kwao, ambazo ni vitu kama uhifadhi wa maji, mipango, kusimamia migogoro kati watumiaji mbalimbali wa maji, Kufuatilia maji, kutoa ruhusa, utaratibu na malipo.
Kufuata miongozo ya sera na kufuata miongozo hii yote ya kikazi kuhusu namna ya kuanzisha taasisi na halafu hiyo ikahusu aina, tuseme mandeleo ya shirika la taasisi likiwa na mhasibu, na akaunti ya benki na mfumo wa uhasibu? Na mikutano ya mara kwa mara na kumbukumbu za hiyo mikutano, n.k. Hivyo huo ni unazishwaji uliorazimishwa kidogo. Na huo mchakato ni mgumu kidogo kwa sababu ya vitu kama ukosefu wa mfumo wa kusomeka kwa tarakinishi,, kwa mfano wa hizi huduma.  Watu hawana tarakinishi za kuandika hivi vitu. Na uwajibikaji pia ni mgumu. Sasa kuna mifumo ya ulipaji kwa simu pia ila hadi sasa, ilikuwa vigumu kidogo kuhamisha pesa taslimu. Na Watumiaji wengi wa Maji, Viongozi wengi wa Miungano wangechukua usafiri wa siku mbili kwenda kwa ofisi ya uwanda.  Hivyo ndivyo chanzo kinavyo kwenda na ada na halafu si lazima kulipwa kwa usafiri na kwa siku wanazotumia kufanya hiki.  Hivyo ni ngumu kidogo kufanya mfumo ufanye kazi bila fedha, na bila ufuatiliaji. 
Kwa ofisi ya uwanda kuamua nani atapewa kibali cha maji au la, wanahitaji kujua hasa maji kiasi gani unachukua, siku gani za mwaka na ili kufanya hivyo, unahitaji kifaa cha kupima! Hivyo ni vigumu sana kujua nani anatumia maji na muda gani na matokeo ya hilo ni kwamba watu walioko juu ya mkondo kwa maana kule juu mto unapoanzia, wanatumia maji kama wanavyotaka, na halafu ukiishia chini ya mkondo, maji ni kidogo zaidi uliyobakiwa nayo. Na hivyo njia mojawapo ya kushughulikia hilo suala ni kukusanya taarifa nyingi kuhusu upatikanaji gani wa maji uliopo kwa muda gani ya mwaka halafu ugawanye kwa idadi ya watu wanaohitaji na kwa muda gani wanahitaji. Ila hiyo taarifa ni nzito sana. 
Na ndiyo sababu ya mfumo huu wa kukusanya taarifa kuwa mzito. Mzito sana kwa mahitaji haya kuhusu namna ya kusimamia maji ni nafikiri imerithiwa kwa mfumo wa kikoloni au shauku ya kaskazini mwa ulimwengu ya ukusanyaji wa taarifa, maamuzi yaliyojikita kwenye taarifa inayotegemea taarifa mahsusi kidogo. 

Olivia: Imekuwa muhimu kuhakikisha wale wenye ufikiaji pungufu wa maji kutokana na kuingiliwa kutoka nje wanafidiwa kwa haki.  Mpango mmoja wa fidia ulihusisha kuanzishwa kwa miradi ya ufugaji nyuki karibu na mto, kama namna mpya ya kipato kwa watumiaji waliopoteza ufikiaji wao wa ukingo wa mto kufuatia mradi wa umwagiliaji unaoanzishwa.
Hivyo, ni vigumu kujua kama aina hizi za miradi zinafanya kazi kweli kwa watu waliyopangwa kufidia. 

Nathalie: Hivyo mipango hii mingi inarudiwa tena na tena katika maeneo tofauti ya nchi. Ila hakika hatuna maoni ya kweli kama hii inafanya kazi kweli kwa watu walioondolewa. Kwa mfano, na wanatengeneza kiasi sawa cha kipato au la? Na hii inakaaje baada ya miaka mitano, baada ya miaka 10?
Hivyo bado kuna maswali wazi kuhusu namna ya kusimamia ubadilishanaji kati ya nini rasilimali ya maji inatoa kiukweli ambayo ni fursa ya kiuchumi, maana ardhi ni fursa sawa ya kiuchumi na uendelevu wa kimazingira.   Halafu hiki kipengele cha usawa maana wale wanaoondolewa ndani ya ukingo wa mto kwa mfano, wataondolewa kwa faida ya mtu fulani chini ya mkondo ambaye ataweza kutumia maji kwa umwagiliaji, tumeseme mwenye vibali.  Hivyo hizo ndizo aina za ubadilishanaji ambazo ni muhimu kujadili, ila hazitambuliki kweli kama ubadilishanaji kwa sababu Usimamizi Jumuishi wa Rasilimali ya Maji inaeleza kuwa inafanya kazi ya kuboresha ufanisi wa kiuchumi, uendelevu wa kimazingira, na usawa bila kutaja hiyo, una ubadilishanaji kati ya hizi “E” tatu (economic efficiency, environmental sustainability).

Olivia: Huu ubadilishanaji zinaathiri watu kitofauti kutegemeana na usuli wao, utajiri, au kama wanaishi mjini au vijijini. Miradi ya umeme wa maji, kwa mfano, mara nyingi ni ya faida kwa watu wa mjini wanaoweza kufikia umeme unaotengenezwa na mabwawa, wakati wakazi wa vjijini wanaweza kubaki bila kuunganishwa kwenye gridi. Jinsia inajalisha, ikimaanisha wanaume na wanawake wanaweza pia kuathiriwa na kitofauti sana na mabadiliko katika upatikanaji wa maji.

Nathalie: Watu wengi wanaoishi pengine katika maeneo haya ya umwagiliaji kama wako vijijini sana, wasingeweza hata kuwa na ufikiaji wa umeme, ingawaje kuna ukweli kuwa wanaambiwa, tuseme au wanajadiliana waachie maji yao kidogo kwa ajili ya uzalishaji wa umeme. Hivyo muda huo utakuwa na ugawaji huu kati ya hawa watumiaji tofauti ili katika viwango tofauti watumiaji tofauti na pia vipaumbele tofauti na hapo ndipo suala la jinsia linaingia kwa nguvu tukichukua mfano mmoja, tuseme kuwa wanawake ni walezi zaidi na wangejali kuhusu afya za watoto wao, kwa mfano, kuhusiana na lishe au kuhusiana na afya ikihusishwa na maradhi yanayotokana na maji kwa mfano, na wanaume wangeweza kuwajibika kidogo kuleta fedha nyumbani, hivyo au chakula. Hivyo wanaume wanaweza kuwa na hofu juu ya kiasi cha maji kwa sababu watukwa wanataka kumwagilia mazao yao, wakati wanawake wanaweza kuwa na wasiwasi juu ya ubora wa maji, kwa sababu hawataki watoto wao wafe kwa magonjwa yanayotokana na maji, kama vile kuharisha. Hivyo kwa namna hiyo, ni muhimu sana kuhakikisha kuwa sauti zote kama tunaongea kuhusu jinsia, kama tunaongea kuhusu aina ya watumiaji tofauti wa maji. Ni muhimu sana kama maoni yote angalau zimeelezwa, halafu zikajadiliwa. Na hiyo imefarijiwa kwa hofu ya haki ya umma, ila mwishoni, pia ni hofu kuhusu ufanisi. Kwa maana ukiwa na mgogoro au ukiwa na uhujumu halafu kila mtu anapoteza hivyo hiyo kidogo. 

Olivia: ingawa kuna magumu haya, kuna baadhi za njia mbele za kuanza kuzishughulikia na kutengeneza mfumo ulio na usawa zaidi, na ambayo pia inahitikia hali zinazo badilika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Nathalie: Kitu kimoja ambacho kimekuwa kigumu kweli ni kuleta huu uzoefu kutoka utafiti na kutoka WWF, ambalo ni shirika lisilo la serikali la utafiti kimataifa, kwa mfano, halafu kuleta hii kwa kazi yangu ya sasa nikifanya na misaada ya nchi mbili, ambayo ni msaada wa serikali kwa serikali kati ya Ujerumani naTanzania, ni kwamba huu uzoefu umekuwa ukiweza kulisha ukuaji wa mawazo ya kivipi tunaweza kufanya vitu vitende kazi kwa uendelevu zaidi, hata ndani ya hii miundo ambayo si kamilifu. 
Ni vizuri kujaribu kuendeleza suluhu kwa ushirikiano. Hivyo bila kuja na suluhu ila kuendeleza suluhu kwa ushirikiano kupitia matendo ya pamoja kati ya sekta mbalimbali. Hivyo sasa kwa mfano, kufanya kazi sana kuhusu ushiriki wa sekta binfasi na ushiriki wa asasi za kiraia ingawaje asasi za kiraia hazijaendelezwa sana Tanzania. 

Olivia: Hivyo unafikiri kuna njia ambayo tunaweza wote kuilinda uhifadhi na pia kulinda riziki? Kwa wakati mmoja inayozunguka usimamizi wa maji? 

Nathalie: Hivyo sina hitikio la hilo kikamilifu kwa sababu nafikiri hakuna ye yote anayo ila nafikiri njia moja ya kwenda mbele, ni kutoka pale, ni kutambua kuwa kuna ubadilishanaji ila pia kutambua kuwa vitu hivyo viwili vina ambatana. Hivyo hatuwezi kuwa na riziki kwa miaka 50 kama tumemaliza rasilimali zetu za asili. Na hatuwezi kuhifadhi maeneo wakati watu wana njaa mlango wa pili. Hivyo kuna hitaji la kutambua kutafuta suluhu ya na hii naipenda, majadiliano kidogo yanaendelea kuhsusu asili, suluhu zinazojikita kwenye asili. Na hivyo kukaa mbali na kipengele cha usasa kuwa kuna ukusanyaji huu mzito wa taarifa, tuseme kwa mfano, kuna hili wazo kuwa usasa huja na miundombinu, kwa mfano, ambacho ni kitu kinaitwa usasa wa juu. Tukikaa mbali na wazo hilo na kuweza kurudi au kwenda kuelekea hili wazo kuwa masuala haya yamejumuishwa na pamoja, tumgeweza pia kuona faida, ya kuhifadhi rasilimali asili, wakati pia tukitengeneza rasilimali ambazo ni endelevu zaidi ili hivi vitu viwili viweze kuambatana. 

Olivia: Kwa Nathalie, suluhu litakuja, ili mradi michakato iliyoundwa kusuluhisha masuala ya maji yanajumuisha sauti za kila mtu katika ngazi za wazawa.

Nathalie: Masuala ya maji hayahusu tu masuala ya maji, yanahusu nani, nani anapata kitu na nani hapati kitu na hicho kimepachikwa kwenye mfumo mpana. Na huo mfumo mpana ni wa nchi ambayo ipo katika nafasi ya chini katika soko la dunia, ni ya nafasi ya, unajua, hadhi ya baada ya ukoloni, imo katika jamii ya mfumo dume na, na, na katika vingine vingi, hivyo kama hatuwezi kuweka mbali mktadha kutoka, kutoka uhalisia na hicho ndicho kimekuwa pia kigumu sana kuhusu majibu ya utafiti ni kivipi unatengeneza mambo ya ujumla kutoka kitu ambacho kilikuwa maalum na hapo ndipo ninapopenda kufanyia kazi kanuni, haswa mtazamo wa haki ya jamii na mazingira, ni kuhusu, vipi mchakato utaboreshwa? 
Nafikiri, hata suluhu haziendelezwi sasa, cha muhimu kuzingatia kwa mtazamo wangu ni michakato. Hivyo mchakato ukiwa na usawa, mchakato, utawala wa mchakato ukiwa na haki, ikiwa watu wana sauti ya kuzungumza ndani yake, n.k. kama kutokuwa na usawa wa mamlaka una fidiwa kama hatuangalii au kuipa kipaumbele tu katika michezo ya kiuchumi, na kama tunaangalia muda mrefu badala ya muda mfupi, hivyo kama kweli tunawajibika kwa vitu hivi  katika mchakato inayo chagiza siku zijazo, basi nafikiri tunaweza kufanya iwe sawa kwa sababu itakuwa maamuzi ya watu wanaohusika na suala, kuwa mjadala kuhusu uhifadhi inafanywa na mashirika ya kimataifa yasiyo ya serikali yaliyoko Kaskazini mwa Ulimwengu umeharibika kwa namna fulani. Kwa sababu, namaanisha, kuna wasiwasi wa haki za jamii. Na wasiwasi wa haki za mazingira ambazo zinawakilishwa katika sehemu hizi, ila nafikiri namna ambavyo ubepari unafanya kazi ni kwamba ina husu faida za kifedha na hayo mafanikio na tukiendelea na hilo, na hilo lengo, nafikiri basi tunapoteza kweli faida za kubaoresha mchakato wa maamuzi, kuelekea matokeo ambazo kwa matumaini yangeweza kuwa yanahifadhi rasilimali asili na kuboresha maisha na riziki za watu wanoishi katika maeneo yote tofauti. 
[AKIZI KUTOKA OLIVIA—sehemu hii ilitafsiriwa kwa kutumia Google translate:
Haya yalikuwa mazungumzo ya kufumbua macho na Nathalie. Kiini cha mazungumzo haya ni jambo muhimu la kuchukua kwamba kuna pengo kati ya sera na mazoezi yanayozunguka usimamizi wa maji.
Shukrani kwa utafiti wa kijamii tumeweza kubaini hitaji la kujumuisha washikadau wote ili kuruhusu uboreshaji wa maisha yote yaliyoathiriwa na usimamizi wa maji.
Pia nilifurahia sana kujifunza kuhusu jinsi athari za usimamizi wa maji zinavyozingatiwa, pamoja na majukumu ya kijinsia kuangazia vipaumbele vya wanaume na wanawake na wasiwasi wa usimamizi wa maji juu ya riziki zao.
Na mwisho, ni muhimu kutafakari juu ya mada zinazojirudia za ukoloni na usasa.
Kwa mara nyingine tena, asante sana kwa Dk. Nathalie Richards kwa ufahamu wake na wakati.]

Asante kwa kusikiliza sehemu hii ya mwisho wa mfululizo wetu. Kama ulikosa sehemu mbili ya kwanza, unaweza kupata katika, pamoja na nakala kwa Kiingereza na kiSwahili ya kila sehemu. Utapata anuani ya barua pepe yetu katika tofuti yetu, au wasiliana nasi kupitia tweeter kwa anuani hii @UCLanthropology.

Katika sehemu yetu ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho Hein Aung atakuwa akiongea na Eva Maria Anyango Okoth, mwanasheria na afisa mwandamizi wa programu  aliyeko shirika lisilo la serikali la haki ya asili, kuhusu kazi yake kutetea mazingira na haki za jamii katika Afrika Mashariki katika uso wa mipango mingi mikubwa ya miundo mbinu.

Ahsante kwa kusikiliza, na tutakuona wakati mwingine!