XClose

UCL Anthropology

Home
Menu

Episode 1: Modernism and the Drive to Dam Swahili Transcript

Mahojiano Ya 1 – Podcast - Hearing Above The Roar – ‘Kusikia Juu Ya Kishindo’

Mhoji: Lily Higgitt
Mhojiwa: Barnaby Dye

L: Habari na karibu kwa ‘Kusikia juu ya kishindo’ podikasiti ya mfululizo ya sehemu tatu  inayo ondoa utata katika sauti inayo endelea ulimwenguni juu ya ujenzi wa bwawa kubwa katika Afrika Mashariki. Katika mfululizo huu, tutachunguza maana ya hii sauti kwa watu wanaoishi katika njia yake.  Mimi ni Lily, mwanafunzi wa Anthropolojia, Mazingira na Maendeleo katika chuo kikuu kishiriki London na ni mwenyeji wako kwa sehemu hii.

Kote katika sehemu hii,tutasikia toka wataalam watatu tofauti, tunapo chunguza kinacho sukuma mabwawa haya. Na tunaangalia sababu kuhusu kwa nini miradi mikubwa ya miundo mbinu ya nishati inaendelea kufanyika bila mipango ya kutosha au fidia kwa wale watu ambao wataathirika zaidi nayo. Leo, tutakuwa tukiuliza kwa nini hii miradi mikubwa inaomba serikali za kitaifa, hasa wakati faida na gharama kwa wananchi wake hazigawiwi kwa usawa.  Katika sehemu yetu inayofuata, tutazingatia namna wapangaji wa mradi wataweza kukutana kwa ufanizi zaidi na kwa haki na watu wanaotegemea rasilimali ya maji kwa riziki zao, na kuongea kuhusu njia ambazo wazawa wanajipanga kufanya sauti zao zisikike kwa serikali. 

Wanafunzi wenzangu Olivia na Hein wataungana nami katika sehemu hii, ambao watakuwa wenyeji wako katika sehemu zinavyo fuata… unapenda kusema habari na kujitambulisha?

Olivia: habari! Hujambo watu wote, mimi ni Olivia, na mimi ni mwanafunzi wa uzamili katika ethnografia na filamu katika UCL, na ninatumahi kuwa podikasti hii itafungua macho yako kuona athari za mabwawa ya kufua umeme kama vile matokeo ya maisha na mazingira na njia tunaweza kuchunguza na kutafiti athari hizo.

Hein: Habari watu wote, mimi ni Hein Aung Htet, mimi ni mwanafunzi wa uzamili katika anthropolojia ya jamii wa chuo kikuu kishiriki London na nilitaka kutengeneza podikasiti hii inayoongozwa na wanafunzi kwa sababu ya umuhimu wa mabwawa ya umeme wa maji na athari zake kwa mazingira, riziki za jamii na mipangilio ya kijamii.  

Lily: Kabla ya kuingia kwenye mahojiano ya sehemu hii, tunataka kukuelezea kuhusu kwa nini tunatengeneza podikasiti hii kuhusu umeme wa maji.

Rob Nixon, katika kitabu chake Ukatili wa Taratibu na Mazingira ya Masikini, imechapishwa 2011, anaandika kuwa: “karne ya 20 ilikuwa ni karne ya mabwawa makubwa: katika 1900, hakuna bwawa katika sayari yetu iliyokuwa na kimo cha mita 15; miaka mia baadaye, kulikwa na mabwawa 36,562 zilizo zidi kimo hicho”. 

Sasa tunaishi katika sayari ambamo mito michache na michache zina furuka kwa bahari. Somo katika Asili mnamo 2019 iligundua kuwa, kati ya mito mirefu Duniani (ile iliyo zidi 1000km kwa urefu) ni theluthi moja tu (au 37%) inabaki kufurika kwa uhuru kwa urefu kamili, mabwawa na hifadhi za maji zikiwa kikwazo katika njia zao.

Olivia: Mwishoni mwa karne iliyopita, kipimo na nafasi ya ujenzi wa bwawa ilikuwa kwamba, katika 1998, kikundi cha watalamu wa kimataifa waliombwa kuhakiki kama mabwawa makubwa yalikuwa yanapelekea ufikiaji wa malengo ya maendeleo kiukweli. Ripoti toka Tume ya Dunia ya Mabwawa iliyochapishwa mwaka 2000 ulitengeneza usomaji mkali. Ilihitimisha kuwa, “wakati mabwawa yametengeneza mchango muhimu na wenye maana katika maendeleo ya binadamu … katika matukio mengi bei isiyo kubalika na mara nyingi isiyo ya lazima imelipwa kuokoa hizo faida”. Lakini bei ilikuwa ni nini? Ni nini kitafanyika mto ukiwekwa bwawa? Umeme wa maji haupaswi kuwa ‘kijani’?

Hein: Umeme wa maji unaweza kufanywa upya, lakini haimaanishi kuwa ni “kijani”. Kiikolojia, mabwawa hutengeneza hifadhi kubwa za maji yaliyotuama na kukatiza mafuriko ya mto. Hiyo ina athari kubwa katika mfumo wa ikolojia na katika uvuvi, na inachangia janga la upoteaji wa viumbe hai miongoni mwa viumbe wa maji safi duniani  

Kijamii, faida za mabwawa yanashirikiwa kwa kutofautiana, mara nyingi kwa kupendelea wakazi wa kiwanda na wa mjini ambao tayari wameunganishiwa gridi ya umeme, badala ya wakaazi wa kijijini ambao riziki zao zimekatizwa na uwekaji wa umeme wa maji. 

Inakadiriwa kwamba watu milioni kati ya 40 na 80 wameondolewa mabwawa makubwa yakijengwa. Karibu bila kubagua, kama Rob Nixon anavyoandika, huu uondoaji hupelekea kudorora kwa ubora wa maisha kwa namna lishe, afya, vifo vya watoto wachanga, umri wa kuishi, na utoshelevu kimazingira. Watu wanaobaki nyuma watakuta mfumo wa kiikolojia umebadilika sana, huku mifumo ya kilimo na uvuvi iliyokabiliana na mzunguko wa majira kudhoofishwa, hivyo kuhatarisha njia za maisha. 

Lily: Kutokana na ripoti ya Tume ya Dunia, taasisi kubwa ya kifedha kama Benki ya Dunia zilionekana kutekeleza wito wake wa kusitishwa kwa ujenzi wa bwawa jipya, na mito ya dunia kidogo ikapumua.  

Hata hivyo, umeme wa maji sasa unashamiri tena, miaka 20 baadaye, na miradi hii mipya inaleta utata wote uliofanana.

Olivia: Muda huo huo, ufikiaji wa taarifa, kupitia simu za mkononi na mtandao, zinatengeneza fursa kwa hata jamii zilizotengwa zijipange na kushirika maamuzi juu ya mabwawa.

Hein: Na hicho ndicho tunachotaka kuangalia katika mfululizo wa podikasiti hii.  Pamoja na kuchunguza sababu za kufufuka kwa umeme wa maji katika kusini mwa jangwa la Sahara mwa Afrika, tunataka kujua kama kuna njia kwa watu kushiriki katika miradi hii ya kimaendeleo, ili kuruhusu matokeo bora ya kimazingira na za kijamii kwa kila mtu. 

Lily: Kuendelea na mada yetu kwa sehemu hii, kuelewa nini iko nyuma ya msukumo huu wa kujenga mabwawa kusini mwa jangwa la Sahara, Afrika. Tutakuwa tunaangalia mfano wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere. Hili ni bwawa la megawati elfu mbili mia moja na hamsini ilioanza kujengwa 2019 katika mto Rufiji kusini mwa Tanzania.

Itakapokamilika, kiwanda kinakusudiwa kutoa umeme maradufu ya ile ya nchi, viongozi wakidai kuwa hii itatoa umeme wa bei rahisi kwa raia, kuendesha treni mpya ya umeme, na hadi kusambaza umeme kwa nchi jirani. 

Hata hivyo, ujenzi umekuwa ukisumbuliwa na uchelewaji wa uwekaji wa mipango na fedha, na kwa sasa inatembea miaka miwili nyuma ya ratiba na bilioni nyingi za dola za kimarekani juu ya bajeti. Hata wanaounga mkono mabwawa katika vyombo vya habari vya Tanzania wanatambua kuwa mradi una kasoro, kwani inategemea ripoti ya upembuzi yakinifu iliyopitwa na wakati na imeendelea bila tathmini yo yote ya athari za kimazingira na kijamii – wazi ni kinyume na mapendekezo ya Tume ya Mabwawa Duniani.  

Lily: Katika sehemu hii, nazungumza na Barnaby Dye, Mhadhiri katika Maendeleo ya Siasa Chuo Kikuu cha York, na mtafiti mwenzetu kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Dunia katika Chuo Kikuu cha Manchester. 

Utafiti wa Barnaby inazingatia kufungua michakato ya kufanya maamuzi, mikakati na itikadi zilizohamasishwa kwenye miradi tofauti za maendeleo na miundombinu; iliyojikita kwenye ukusanyaji wa takwimu kule Ghana, Ethiopia, Rwanda, Tanzania, India na Brazil. Tumemleta kwenye maonyesho leo ili kuelekeza baadhi ya utata na ugumu kwenye mradi wa bwawa la Nyerere lililoko Rufiji, Tanzania. Kwa Barnaby, miradi ya umeme wa maji inatoa utambuzi kuhusu namna maendeleo inavyofanyika katika hali halisi kwenye ngazi nyingi za jamii.

BD: Mara nyingi wanahusisha vipande vikubwa vya miundombinu za kuleta mabadiliko na vipengele vingi sana za nini kinahusishwa katika kuweka pamoja mradi wa miundombinu kama ile kama ni upande wa fedha au siasa za jiografia au kwa athari kubwa tu kwa mifumo na mifumo inayounga riziki za watu na inayoweza kubadilisha kiukweli njia yao ya maisha. Hivyo hiyo inakuruhusu sana uulize maswali kuhusu kusanyiko mzima wa siasa za kimataifa, kitaifa na kieneo. Muundombinu ni kitu muhimu na umeme wa maji ni kitu muhimu sana kitakachokuruhusu kuleta vitu hivi vyote pamoja.

Lily: Tulipoanza kwa mara ya kwanza kupanga mfulullizo huu, mpango wetu ulikuwa ni kuzungumza na wataalamu, kama vile wewe, lakini pia kusikia toka watu ambao wanaathiriwa moja kwa moja na bwawa pendekezwa la Nyerere, kwa kuzungumza kwa watu wanaoishi na jamii zinazoishi pembezoni mwa Mto Rufiji, na wafanyakazi tendaji wa shirika lisilo la Serikali katika eneo. Lakini, kiukweli haikufanya kazi kama tulivyotegemea.…

Hivyo bwawa la Nyerere limeonekana kama kifani bora ya kuchunguza masuala haya yenye utata kati ya faida zilizoahidiwa ya umeme wa maji na matokeo hasi yaliyotarajiwa. Pia tuna uhusiano na watu wanaoishi Rufiji, kupitia utafiti uliyofanywa awali na idara yetu ya anthropolojia.

Hata hivyo, katika kuunganishwa pokasiti hii mapema tuligundua kuwa kuomba maoni toka Watanzania- hata kwa wataalam wanaofanyia kazi Mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali– na kurekodi, inaweza kuweka watu katika hali ya wasiwasi, kama si ya hatari. Kwa nini unafikiri watu wanasita kuwa wakosoaji wa mradi?

BD: Tanzania imechukuwa upande wa kimabavu, lakini mara nyingi imekuwa ni nchi ambayo ningeweza kuelezea kama, vizuri, toka uanzishwaji wa demokrasia, haijawahi kuwa nchi ya demokrasia ya kweli kama tunavyoelewa katika muktadha wa Uropa/Marekani ukitaka.  Na kuhusu hilo namaanisha hakujawahi kuwepo kiwango sawa cha uhuru wa vyombo vya habari au uwezo wa kuandamana, hakuna kile kiwango cha haki za raia tunayohusisha demokrasia hapa.  Na kwa hiyo nafikiri imeeleweka kwa upana kuwa ni hatari kuzungumza moja kwa moja dhidi ya serikali. Na nafikiri mara nyingi hivyo ndivyo imekuwa uhusiano wa Tanzania na demokrasia, ambako kuna wazo lenye nguvu la baadhi ya kanuni za demokrasia na kuheshimu sauti toka chini lakini zinapaswa kutoka ndani ya nchi na zinatakiwa zisiwe za kuleta changamoto. Na hivyo basi nafikiri kuwa kwa mtu huru, kama huyo, ni Mtanzania au mtu kutoka nje ya nchi, kuja kuuliza haya maswali na kujaribu kukusanya maoni hayo, hiyo mara nyingi itatazamwa kwa mashaka makubwa kidogo. 
Kama wewe ni mwandishi wa habari au mwanataaluma anayejaribu kuelewa au anayejaribu kwenda zile sehemu, ambazo bila shaka zinafanya iwe ngumu kwa sababu ili uende pale unapaswa upitie hawa walinda malango wanaodhibitiwa na chama na kudhibitiwa na nchi, na hivyo kufanya utafiti katika mktadha ule inaweza kuwa ngumu kweli. Hivyo unapaswa uwe unafanya utafiti ambao nchi iko sawa wewe kuufanya, na bila shaka nchi inaelewa, kwa kiwango fulani kuwa huu mradi unaweza kuwa na utata kwa watu hawa, na hivyo inaweza ikawa na athari hasi kwa baadhi ya watu wale na kwa hivyo haitakuwa tayari kuwaruhusu kutembelea kwa uhuru na kuzungumza nao.
Ikiwa mgeni katika eneo kama sisi, utafiti wa Barnaby na ukusanyaji wa takwimu ndani ya Tanzania na katika nchi zingine katika eneo, mara nyingi kufanya kazi pamoja na watafiti wa ndani ya nchi, inamsaidia kuzungumza kuhusu historia ya ujenzi wa bwawa. Vile vile kuhusu baadhi ya masuala pembezoni mwa umeme wa maji katika Afrika Mashariki leo. 

Barnaby amejifunza simulizi inayojirudia ya kisasa na maendeleo iliyohamasishwa kwa bwawa la Nyerere na Mradi wa Umeme wa maji wa Maporomoko ya Rusumo katika mpaka wa Tanzania-Rwanda. 

Kama miradi mingi ya ujenzi wa mabwawa katika Afrika, zina historia ngumu kwa vyama vingi tofauti vinavyohusishwa katika mipango na ujenzi. Mara nyingi, mizizi ya historia hiyo imetoka ukoloni. Na bado leo, ni taasisi za kimataifa na serikali za nje ndizo zimekuwa zikifadhili ujenzi wa mabwawa katika eneo lote.  

BD: Sababu ya wao kutaka kufanya hivyo imebadilika toka muda. Kwanza kulikuwa na hisia kwamba mabwawa yanacheza nafasi kubwa katika kazi za maendeleo ya kimataifa na uanzishwa wa nchi hizi huru baada ya uhuru toka kwa ukoloni. Nafikiri hivi karibuni kumekuwepo zaidi ya maslahi katika mabadiliko ya tabia nchi na mabwawa na umeme wa maji kama njia ya kupata maji, ambayo ni njia finyo ya kuelewa usalama, nafikiri. 
Kuna pia serikali ya kitaifa kiaina katika upande mwingine wa shilingi, ambao wana maslahi na mabwawa na nafikiri kufuatilia maslahi yao kama kutoka ukoloni kuendelea mizizi mingi ya hiyo imetoka kipindi cha ukoloni. Katika kipindi kilichopita cha ukoloni kutoka miaka ya 1930, 1940, 1950, 1960, kutegemeana na kipindi zilipata uhuru, kulikuwa na nia ya kusimamisha uchumi wa nchi hizi na kuendeleza hizo nchi zaidi kidogo na hii mara nyingi ilifanywa kwa njia ya kuwafanyia watu maamuzi lakini kulikuwa na msukumo wa maendeleo kwa kiwango. Na mabwawa yakawa kifaa muhimu kidogo kwa msukumo huo kwa sababu zote utakazo tegemea. Wangeweza kufungua mashamba makubwa ili baadaye wauze bidhaa kule Uropa au wangeweza kutengeneza umeme ambao ungeweza kunyanyua viwango vya viwanda na kusaidia watu wa mjini.  Na hivyo unaona katika muktadha wa Afrika kipekee aina ya kwanza ya mabwawa makubwa inaanza kujengwa katika kipindi hiki na pengine mfano wa kuwakilisha mabwawa ni bwawa Kariba katika Mto Zambezi ulioko Zimbabwe/Zambia ambapo kwa sasa ndipo mpakani mwa Zimbabwe na Zambia. Na nyingi za mawazo yaliyofanana na hayo yahusuyo maendeleo huwa zinachukuliwa na viongozi wa uhuru na hivyo ingawaje labda baadhi ya masomo yalianzishwa chini ya kipindi cha ukoloni viongozi wengi wa uhuru walichukua mawazo ya hii miundo ya juu-chini ya maendeleo ya kuleta usasa na kwa hivyo uliona msukumo ulioendelea kuhusu ujenzi wa mabwawa baada ya uhuru umekuwa na nguvu hata baada ya nchi kupata uhuru. 

Lily (katika mahojiano): katika maktadha wa kutaka kuondoa ukoloni katika maendeleo, nafikiri inavutia pia namna hizi serikali zinavyosukuma miradi kama mabwawa makubwa ambazo nazo zimehusishwa na ukoloni lakini kwa namna ya baada ya ukoloni. 

BD: Ndiyo na kuna kuhama kwingi unaotokea katika ukoloni huu hadi kipindi cha baada ya ukoloni kwa namna ambavyo hii miradi inafikiriwa, kusudi lao linaenda kuwaje na mawazo kuhusu nini kinawezekana kwa sababu yao. Nafikiri katika kipindi cha ukoloni hiyo imekatazwa zaidi na kabisa imepachikwa kwenye mawazo ya ukoloni unaoendelea. 
Hivyo bila shaka katika nyakati hizi si kuhusu ukoloni unaoendelea lakini basi imeandaliwa kwa njia tofauti hivyo sasa itatumiwa kwa mawazo ya viwanda, ya kunyanyua hizo uchumi, ya kuwapa watu ajira, lakini mwishoni bado ni teknolojia ndiyo ina gharama hizi kubwa. Inakuaga na faida kubwa pia ila gharama kubwa pia zipo na hivyo inavutia namna mawazo haya ya usasa wa maendeleo yanahama.  

Lily: Bwawa la Nyerere ni mfano unaoeleweka kuhusu mizizi ya ukoloni na itikadi zinazotawala ya maendeleo zinaweza kuendelea kuendesha ujenzi wa miradi ya mindombinu kiwango kikubwa katika ulimwengu wa leo wa ukoloni mambo leo.  

BD: Hivyo nafikiri mradi huu unatoa muhtasari mkubwa wa nini tumekuwa tukiongelea. Ina kipengele cha nguvu cha utegemezi wa njia. Mantiki ya kuanza kuzamisha hela katika kuendeleza mradi, ukianza kuzamisha hela katika mipango, kusoma na kufanya kazi maandalizi ya uhandizi ya kujenga mradi basi itabidi iendelee kuzunguka na ni ngumu sana kuiachia. Na kwa mradi huu unaweza kufukuzia… Imekuwa ikiitwa bwawa wa korongo la Stiegler na hii ni kwa sababu kwa mara ya kwanza ilitambuliwa kama eneo lenye uwezo wa kuwekwa bwawa na mhandisi wa kijerumani mwanzoni kabisa mwa karne ya 20 bila shaka likiwa koloni la Wajerumani. Hivyo ina historia hii ndefu, imejulikana kama eneo la bwawa kwa muda mrefu. likiwa ni koloni la Waingereza kulikwa na mafunzo mengine zaidi yaliyofanyika, Mashirika kama UN for Japanese Aid Agency, US AID, FAO zote ziliweka mafunzo kwa bwawa hili katika vipindi tofauti. Yote yalichukuliwa kwa kiasi kikubwa zaidi na Wakala wa Maendeleo ya Norwe katika miaka ya 1970/1980.
Historia hiyo yote inaipa mradi kuendelea, hata ikiwekwa pembeni kwa vipindi tofauti katika historia yake na kukataliwa bado itaendelea kuwepo, bado ipo kwenye rafu. Hivyo serikali mpya yenye pesa kidogo ikiingia madarakani, yenye nia fulani zaidi, ambayo inajaribu kufanya maendeleo Tanzania unanyanyuliwa kama mradi mmoja unaoeleweka kama una nguvu kubwa nchini. 

Lily: Mara ya mwisho mipango ya bwawa la korongo la Steigler iliwekwa pembeni,1984, kwa sehemu kubwa ni kutokana na jitihada za utafiti wa kundi la Watanzania na watafiti kutoka nje walioko Chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania, ambao kwa kiini, ndio sauti ya wakazi wa bonde la mto.
Lakini kama Barnaby ataendelea kutuambia, mipango ilikuwepo kwenye rafu, na Jakaya Kikwete, ambaye alikuwa rais wa Tanzania kutoka 2005 hadi 2015, anaamua kuikung’utia mbali. 

BD: Haswa kuelekea mwishoni mwa awamu yake/mwishoni mwa awamu ya pili kulikuwa na msukumo mpya wa kujenga bwawa na hii ni kwa sababu nchi ilianza kuendelea kiuchumi kulikuwa na pia na ukuaji mpana wa uchumi uliokuwa ukiendelea Afrika kwa sababu ya mzunguko wa bidhaa  ambapo bidhaa kiukweli zilikuwa zinapanda, kulikuwa na pesa nyingi kidogo kwenye mzunguko, kulikuwa na simulizi zenye nguvu ya Afrika kama bara le fursa. Na katika mktadha huu Kikwete anageukia mradi huu kama moja ya miradi mingi ya umeme inayoweza kuongeza uwezo wa Tanzania wa kusakinishwa. Hivyo hiyo ndiyo sehemu kubwa ya historia kuhusu utegemezi wa njia na hii imani ya kuendelea kuwa bwawa hili maalum, bwawa la korongo la Stiegler au bwawa la Julius Nyerere litakuwa chombo muhimu kwa Tanzania, itakuwa funguo la maendeleo, itawawezesha kuruka kutoka daraja hili la chini la mapato hadi kuwa katika nchi ya daraja la kati kwa mapato, itawapa ukuaji wa kiviwanda. Hiyo ndiyo sehemu muhimu sana ya simulizi.
Na Magafuli alipoingia madarakani mwaka 2015 alichukua hii zaidi hata  na hii ikawa hata sehemu yenye nguvu na kwake kweli ikawa kibendera.   Chini ya Kikwete ilikuwa moja ya miradi iliyokuwa ikizingatiwa, Kwa Magufuli hii ikawa bendera inayokwenda kutoa programu zake na matumaini yake ya kuwa Tanzania iliyoendelea zaidi kiumi.    

Lily: Kutokana na hatari za raia wakitanzania kuzungumza kwa uwazi kuhusu maoni kwa bwawa, nilimwomba Barnaby kama angeweza kutupa hisia zake kuhusu athari zinazoweza kutokana na bwawa, kutokana na ufahamu wake wa eneo, muunganiko wake na watafiti wazawa na uzoevu mpana na miradi inayofanana na hii katika bara la Afrika.      

BD: Kutoka ripoti ya UNESCO inaonekana kuwa mchakato wa ujenzi una athari hasi kwa hifadhi. Na hivyo kweli kwa wale wanaohusika na utalii kule na wale wanaohusika na uhifadhi hii ni wasiwasi.
Lakini kwa miradi mingine kila mara nimekuwa nikivutiwa na majibu mchanganyiko ambayo watu mbalimbali wamekuwa nayo kuhusu bwawa. Tofauti kidogo ni kwamba bwawa la Julius Nyerere litakuwa na aina zaidi ya athari za kuwepo kwa wale walioko chini ya mkondo kuliko miradi niliyowahi kuangalia. Kuna hamu ya kukubali kabisa simulizi zenye matumanini zaidi kuhusu mradi, na hayo inaeleweka sana kwa sababu bila shaka watu wengi wanataka kuwa na umeme na kutaka wawe na pengine riziki salama zaidi. Na hivyo kama wanaambiwa kuwa mradi huu utatoa hiyo basi kutakuwa na nyingi kwa jamii ambayo watakaribisha mradi kama ule. 
Lakini basi ni dhahiri kuwa itakuwa ngumu ikiwa muunganisho unaweza kufanywa kwa faida walizonazo ambayo wangeweza kuwa wanapoteza na kwa mfumo wa  huduma za ikolojia kutumia fungu la maneno ya kiufundi ya kimasomo ambayo inamaanisha huduma zinazopatikana kutokana na mto na kwa eneo ambalo linaweza pata mafuriko au ile ambayo inaweza kubadilishwa na namna ambayo unabadilisha mto,  kama kuhusu urutubishwaji, kama inahusu usafishwaji wa mabwawa chini ya korongo na mafuriko ya mwaka, kama inahusu kumwagilia eneo kwa mafuriko ya mwaka. Na hivyo mara nyingi kuna aina ya majibu mchanganyiko ya awali ambapo utapata baadhi ya faida zikiongelewa na kutamaniwa, na kwa matukio mengine ukosoaji mwingi zaidi na basi bila shaka likija uhamishwaji tena utakuwa na mfuko mchanganyiko. Kama mpango wa fidia ukifanywa, basi kutakuwa na baadhi ambao wangeweza kuwa wamefaidika kutoka mpango huo wa fidia na kuwa bora zaidi. Lakini kila mara kuna uwezekano, hata kama mpango wa fidia inafanyika vizuri kiasi, hakuna uwezekano kabisa kutofanyika kwa njia ya ushirikishwaji mkubwa na watu mara nyingi kwa hivyo watapuuzwa.  

Lily: Hivyo ni nini shida kwa mabwawa makubwa yanayoendelea kujengwa? Je yana gharama hasi ya kijamii na kiikolojia bila ubishi? Na kama ndivyo, kwa nini bado yanaagizwa?   

BD: Nafikiri inavutia kuna ongezeko la makubaliano hususan wanasayansi wa kijamii na namaanisha kama unaenda kujumlisha sana asasi za kiraia ulimwenguni na mashirika yasiyo ya kiserikali kuwa mabwawa yana athari hizi hasi nyingi na kwa kweli zinatakiwa zizingatiwe. Lakini hiyo haijawahi kugawanywa kwa wote. Hivyo tunaweza kujadili katika msimamo wa kitaaluma kama unatoa maelezo ya jumla ya fasihi kuna makubaliano ya wazi ya hizi athari hasi. Na makubaliano hayo yaliakisiwa kweli kwenye Tume ya Mabwawa Duniani iliyochapishwa 2000 na kweli kuwekwa kwenye kumbukumbu kwa njia pana zaidi. Lakini Tume ya Mabwawa Duniani ilikuwa pia inavutia maana iliyoonyesha kuwa kulikuwa na kundi la watu waliokuwa wakifadhili mabwawa na kujenga mabwawa na bila shaka wana maslahi waliyokabidhiwa ila pia watu wanaohusika kwenye maendeleo kwa upana zaidi lakini ambao bado kweli waliamini kuwa huu ulikuwa mradi wa miundombinu au aina ya miundombinu au chombo cha maendeleo kitakachowasilisha.   
Na nafikiri kuwa uliona aina ya uvumbuzi mpya wa mabwawa kuzungukia hali ya hewa katika karne ya 21 tu au katika muongo uliopita. Na sasa kuna msukumo mkubwa na labda inakua hata kujenga mabwawa kwa sababu ya hitaji la kufanya badiliko la nishati inayoweza kufanywa upya.  Na ukiwa na fedha nyingi zilizotengewa kufanya kitu na kuna hitaji hivyo la kufanya mradi kuendelea kwa ufanisi na mambo yafanyike na kuonyesha kuwa unatenda hivyo. Inadai pesa nyingi, hivyo inaweza kumaliza bajeti yako, na inazalisha umeme mwingi wa maji na ina huduma baadhi muhimu ambazo watu wanathamini kwa namna ambayo ni ya kuweza kuleta usawa kati ya jua na upepo ambazo bila shaka zinaweza isiwe ya kufululiza na unaweza kuzipa usawa kwa kutumia umeme wa maji. Hivyo nafikiri tunaona tu uvumbuzi mpya wa umeme wa maji, ya kwa nini mabwawa ni kitu cha kujali na kwa nini ni muhimu, na kutoka upande wa wafadhili kuna msukumo kweli ili tu kufanya hii miradi ifanyike. 
Na halafu kama nilivyokuwa nasema kwa upande mwingine, kutoka kwa wapokeaji na serikali za kitaifa ambazo pia zinahusika kusukuma hii miradi nafikiri bado tu kuna si kwa wote ila kwa baadhi ya serikali ambazo ni wapinzani wakubwa. Kuna wazo wa maendeleo ya kimstari sana kuhusu kuwa na umeme na kuwa na viwanda na kuwa na ukuaji wa kiuchumi na si lazima iwe kufikiri namna ya kupita kuanzia A hadi B. Inadhaniwa kuwa kidogo ni uhusiano wa moja kwa moja bila kweli kuzitenganisha hatua ambazo maendeleo ya kiuchumi inahitaji.  

Lily: Ni wazi kuwa kuelewa athari za miradi ya mabwawa kama bwawa la Nyerere ni kitu ila rahisi! 

Kutoka gharama na faida za uchumi, hadi matokeo ya kijamii na athari za kimazingira, mabwawa si suluhu rahisi ya kuleta maendeleo ya kiuchumi kama ambavyo imekuwa ikitangazwa. Ukiongeza hali ya hewa inayobadilika kuwa mchanganyiko na hiyo mvua katika Afrika Mashariki inaongezeka kuwa si ya uhakika, inakuwa hata si wazi kama mabwawa yataweza kuhitikia mahitaji ya nishati ya wazawa, iwapo kiwango cha maji inashindwa kufikia viwango vinavyo tarajiwa.
Kwa kuzingatia ugumu huu na kutokuwa na uhakika, kwa nini hizi simulizi rahisi (kwamba kujenga mabwawa bila kuepukika italeta usasa na ustawi) zinaendelea na kwa nini zinaendelea kuwa na nguvu na kuwa na fedha za kisiasa hadi siku hii? 

BD: Ndiyo, hilo ni swali zuri sana. Nitalijibu kwa njia tatu. Kwanza, kwa sababu tu ni rahisi kupata suluhu rahisi ila siasa hasa kama unataka kushawishi umma, kama unataka kupata uhalali kama kiongozi kila mara kuna hitaji la kuwasilisha vitu haraka na kila mara kuna hitaji la kusema hadithi kuhusu namna kile unachofanya inaenda kusaidia watu waliokusaidia. Na hivyo nafikiri kila mara kuna aina ya shinikizo la kutunga simulizi rahisi kiasi kuhusu baadhi ya maaamuzi haya makubwa.  Na nafikiri hicho ni kipengele kwa hiyo ni  kwa nini baadhi ya hii miradi inaandaliwa kwa njia rahisi kidogo kama za kimaendele na zenyewe bila kujali athari au faida.
Lakini ni ngumu zaidi kuliko hiyo. Ni ngumu zaidi maana si wanasiasa tu katika hotuba za umma wanaotoa aina hizo za balagha na kutumia hiyo aina ya uandaaji. Lakini pia utakuta kwa wapanga mipango ya kiufundi wengi na wahandisi ambao wanahusika katika ujenzi wa bwawa au wanaoamua kufadhili kama ni Benki ya Dunia au Matumizi ya Nishati Tanzania au watumishi wa kiraia Brazil. Na naweza tu kuelea hiyo kwa kujaribu kuchukua mawazo watu walizonazo kwa makini na kwa hivyo sema, vema, kuna itikadi ya maendeleo hapa, kuna itikadi inayosema maendeleo maendeleo kimsingi ni mchakato wa kuchukua watu ambao kwa njia moja au nyingine wanaofikiriwa kuwa wako nyuma kwamba ni wasiostaarabika, hawana razini ya kutosha, wanahitaji kubadilishwa, na kwa hivyo nchi ya sasa ni mojawapo ya makazi zaidi iliyofanywa miji,    ya kuwa na aina hizo zote za huduma za kisasa, na yote ni kuhusu kufikiri tofauti. Na kuna historia ndefu ya miundombinu inayotekeleza jukumu kuu katika kuwaslisha hiyo. Au kuona miundombinu kama inatekeleza jukumu kuu kuendeleza hiyo.
Na nafikiri kuwa mabwawa kipekee yana nguvu sana kwa sababu ya kiwango cha ubadilishaji yaliyonayo. Hii si kuhusu miundombinu peke yake, hii inaweza kuwa kuandika upya bonde lote, ya kubadilisha njia ambayo mto unapita, na hivyo kubadilisha uwanda wote wa mafuriko. Na mahsusi, kuna uwezekano kwa riziki za watu kule. Na inakupa muda huu wa uhandisi wa kijamii ulioenea ambao nafikiri unapendekeza wazo hili la maendeleo kama mabadiliko ya msingi kutoka kwenye maendeleo kidogo hadi usasa. Hivyo si tu kuhusu ukweli kwamba unadhibiti wa mto, ni kwamba unaweza kuwasilisha, au kwamba tu unatengeneza umeme. Ni kwamba unaweza kimsingi kubadilisha njia ambayo mtu anaishi na njia jamii na uchumii zinafanya kazi. Na hivyo nafikiri kuna aina ya huu uvutiaji wa bwawa kwa aina hiyo ya kufikiri, kuna njia ambayo ni mojawapo ya teknolojia chache ambazo zinakupa kiwango hicho cha uwezekano.  

Lily: Shukrani nyingi kwa Barnaby kwa kuchukua muda kuzungumza nami. Kazi yake inafafanua itikadi za msingi za maendeleo, kisasa na maendeleo iliyoko nyuma ya marudio ya homa ya mabwawa ya hivi karibuni. Baada ya kuzungumza na Barnaby, tunakumbushwa kuwa kilichotulia ndani ya simulizi hizi na mijadala kuhusu siku zijazo ni urithi wa kikoloni na historia ndefu za mapambano ya kisiasa. Sababu kubwa kwa nini mabwawa makubwa yanaendelea kushindwa kutimiza maendeleo endelevu ni namna mara nyingi yanavyowasilishwa kutoka mbali na wageni wenye ushirikishwaji mdogo wa jamii za wazawa au hamna kabisa. Pengine muhimu zaidi, nimeachwa na swali lisilovumilika ya ni nini jukumu sahihi ya watafiti wa nje na kwa vipi tunaweza kuangaza wale walioondolewa moja kwa moja au kuathiriwa na ujenzi wa mabwawa makubwa bila kurahisisha mitazamo yao au kuzungumza tena kwa niaba yao.  

Katika sehemu inayofuata, tunachunguza namna watafiti wanavyojaribu kupitia baadhi ya simulizi zilizotawa na changamoto za kisiasa tuliojadili na Barnaby katika miradi ya usimamiaji wa maji   Tanzania. Tutasikia kuhusu michakato ya ushirikishwaji iliyobuniwa kuweka sauti za wazawa ndani ya miradi ya maendeleo, na baadhi ya changamoto iliyohusishwa na kuhakikisha hicho kinafanyika.